0%
HABARI
⟳ Inapakia maujanja...
246
ONLINE
INAINGIA 246...
00 00 00 00 00
MENYU // 246 ONLINE
Nyumbani AI HUB TZ Maujanja Kuhusu Wasiliana Faragha
SYS:ONLINE
SIGNAL
246CORE:v7.0
TZ//DAR
246
246 ONLINE APPSakinisha sasa kupata maujanja zaidi!

Simu 5 Kali za Smartphone Chini ya Laki 2 na Nusu (Tsh 250,000).

 

Utangulizi

Je, unatafuta smartphone mpya lakini bajeti imekaza kidogo? Usijali! Siku hizi, teknolojia imekua sana na huna haja ya kutumia mamilioni ili kupata simu janja (smartphone) inayoweza kufanya mambo yote ya msingi.

Kwa Tsh 250,000 au pungufu, unaweza kupata simu yenye uwezo wa kuingia WhatsApp, Instagram, TikTok, kupiga picha safi na kukaa na chaji siku nzima.

Katika makala hii ya 246 Online, tumekuchambulia simu 5 bora zaidi unazoweza kununua Tanzania kwa sasa chini ya laki mbili na nusu.



Mambo ya Kuzingatia Kabla Hujanunua

Kabla hatujaenda kwenye orodha, hakikisha simu unayonunua katika bei hii ina sifa hizi za chini (Minimum Specs):

01. Storage: Angalau 32GB au 64GB (kuhifadhi picha na video).

02. RAM: Angalau 3GB au 4GB (ili isistak wakati wa kutumia).

03. Betri: 5000mAh (ili idumu na chaji).

04. Mtandao: 4G (kwa internet yenye kasi).


Orodha ya Simu Bora Chini ya 250,000 TZS

1. Itel A70 (Mfalme wa Storage)



Hii ndiyo simu inayozungumziwa sana mtaani kwa sasa. Itel A70 imevunja rekodi kwa kutoa sifa kubwa kwa bei ndogo sana.

Sifa Kuu: 
Storage kubwa ya 128GB au 256GB kwa bei chee.
Kioo: 
6.6 inch HD+
Betri: 
5000mAh (Type-C).
Bei: 
Inapatikana kati ya Tsh 210,000 - 240,000 (kulingana na ukubwa wa storage).

Kwa nini uinunue: 

Kama unapenda kuhifadhi video na picha nyingi bila kufuta futa. (Haujali brand)

2. Samsung Galaxy A04e / A05

Kama wewe ni mtu wa kupenda brand kubwa na unataka simu inayodumu, Samsung ndio jibu. Hizi ni simu za "entry-level" kutoka Samsung.




Sifa Kuu: 
Kamera nzuri na uimara wa brand ya Samsung.
Storage: 
32GB/64GB.
Betri: 
5000mAh.
Bei: 
Tsh 230,000 - 250,000 (Zingatia matoleo ya GB ndogo ili kukidhi bajeti).
Kwa nini uinunue: 
Unataka simu itakayodumu muda mrefu na isiyo na matatizo ya mara kwa mara.

3. Infinix Smart 8

Infinix wameboresha sana muonekano wa simu zao za bei rahisi. Smart 8 inakuja na muonekano kama iPhone na ina "Magic Ring" (sehemu ya juu ya kioo inayoonyesha notifications).



Sifa Kuu: 
Kioo ang’avu chenye 90Hz (Smooth scrolling).
Kamera: 
13MP Dual AI Camera.
Betri: 
5000mAh.
Bei: 
Tsh 220,000 - 245,000.
Kwa nini uinunue: 
Kama unapenda simu yenye muonekano wa kisasa (Stylish) na screen nzuri.

4. Xiaomi Redmi A3

Xiaomi wanajulikana kwa kutengeneza simu ngumu. Redmi A3 ina muonekano wa kioo kwa nyuma (Glass back design) unaoifanya ionekane ya gharama kubwa kuliko bei yake.



Sifa Kuu: 
Muonekano wa hadhi ya juu (Premium Design).
Kioo: 
6.71 inch (Kubwa sana kwa kuangalia movie).
OS: 
Android 14 (Go Edition).
Bei: 
Tsh 215,000 - 235,000.
Kwa nini uinunue: 
Kama unataka simu inayoonekana "Classy" kwa bei ya kawaida.

5. Tecno Spark Go 2024

Hii ni mbadala mzuri wa Infinix Smart 8. Tecno ina soko kubwa Tanzania na spea zake zinapatikana kirahisi.



Sifa Kuu: 
Spika mbili (Stereo Speakers) kwa ajili ya mziki mzuri.  
Storage: 
64GB + 4GB RAM (Extended).
Betri: 
5000mAh yenye chaji ya haraka (10W).
Bei: 
Tsh 200,000 - 230,000.
Kwa nini uinunue: 
Simu nzuri kwa matumizi ya kila siku na kusikiliza mziki.

Hitimisho

Kupata simu nzuri haimaanishi lazimauvunje benki. Simu kama Itel A70 inakupa storage kubwa, wakati Samsung A05 inakupa uimara. Chaguo linabaki kwako kulingana na nini ni muhimu zaidi kwako—storage, kamera, au brand?

Angalizo: Bei hizi zinaweza kubadilika kulingana na duka unalonunulia (Kariakoo vs Mikoani) na kubadilika kwa thamani ya shilingi.

Je, wewe unatumia simu gani kati ya hizi? Tuandikie kwenye comment hapa chini!

Tembelea 246 Online kila siku kwa habari na maujanja zaidi ya teknolojia.

SOMA ZAIDI BONYEZA HAYA MANENO HAPA CHINI.....

SIMU ZINAZODUMU ZAIDI

SIMU ZA BEI GHALI ZAIDI

Imeandikwa Na
Guyashi 246
🔓 ANGALIA
UDUKUZI
🔓 MAUJANJA

Gundua maujanja yetu bora ya simu, kompyuta na intaneti. Yote bure, yote kwa Kiswahili!

246 Online App

246 ONLINE APP

Sakinisha app yetu bure kupata maujanja haraka bila kufungua browser!

Haraka Zaidi
🔓 Maujanja Mapya
📲 Inaona Offline
🔔 Taarifa Mara Moja

🔒 Salama kabisa — Hakuna data inayochukuliwa